Ziwa la maji ya rangi ya waridi AustraliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZiwa la maji ya rangi ya waridi Australia
Ziwa moja la maji ya chumvi mjini Melbourne Australia limegeuka na kuwa na rangi ya waridi kutokana na mwanga wa jua, joto na mvua chache.
Maafisa wa mbuga za wanyama pori wamesema kuwa mwani unaomea katika ziwa hilo chini ya bustani ya Westgate hutoa rangi nyekundu.
Furahia mandhari lakini nawashauri kutoshika maji hayo,alisema victoria.
Ziwa la rangi ya waridiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZiwa la rangi ya waridi
Hali hiyo pia hutokea katika eneo la salina Torrevieja katika ziwa la Dusty Rose na ziwa la Retba nchini Senegal.
Mwanasayansi wa maswala ya kuhifadhi katika bustani ya Victoria amesema kuwa rangi hiyo imesababishwa na mwani kwa jina Dunalliela.
''Sisi hupata maoni kwamba bustani hiyo huonekana kana kwamba ni kiwanda cha rangi kilichomwaga rangi hiyo kwa bahati mbaya''.
Bustani ya victoria nchini AustraliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBustani ya victoria nchini Australia
Dkt Norman amesema kuwa ijapokuwa maji hayo sio hatari ,hangemruhusu mtu kuogelea.
Wasimamizi wa ziwa hilo wamesema kuwa wanataraji kwamba ziwa hilo litabadilika na kuwa yangu yake ya kawaida wakati joto litakapokwisha na mvua kuongezeka.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top