Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa anafahamu watu wanamshangaa kwa sababu alishawahi kusema hatoteua kiongozi wa upinzani katika serikali yake, lakini tayari ameshateua kadhaa.
Rais amesema kuwa, ni lazima watu waelewe maneno hayo alizungumza akiwa mahali gani, aliyazungumza kwenye mkutano wa hadhara Zanzibar.
“Lakini siku zote nimekuwa nikisistiza, Tanzania kwanza. Of course wapo wengine wanaosema, mbona ulishangumza, hutashirikiana, sitateua mpinzani! Ni lazima watu waelewe nimezungumza hivyo mahali gani, nilizungumza nikiwa Zanzibari.”
Rais Magufuli aliyasema hayo mapema leo asubuhi alipokuwa akimuapisha Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Rais amempongeza kiongozi huyo, akisema yeye ni mstaarabu na ni mtu anayejielewa hivyo anafahamu kabisa kuwa nafasi hiyo aliyompa ataweza kuitumikia vyema.
Wakati huo huo, Rais Magufuli alisema kuwa, wapo wabunge wa CHADEMA ambao wamekuwa wakimuomba awateue lakini yeye amewakatalia kwa sababu anataka upinzani uendelee kuwepo.
==>Msikilize hapo chini
Chapisha Maoni