Latest

04:03 AM MMETHALI

KenyaHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionTimu ya Gormahia ya Kenya
Gor Mahia imekuwa timu ya pili ya Kenya kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.
AFC Leopards ndiyo timu ya kwanza ya Kenya kufuzu nusu fainali baada ya kuishinda Singida United na itacheza na Yanga hatua ya nusu fainali.
Gor Mahia imefuzu baada ya kuitwanga Jang'ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere ndiye mfungaji wa mabao yote mawili katika dakika ya 66 na 78. Sasa Gor Mahia wanasubiri mshindi kati ya Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya pia ambao umeanza tayari.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
07 Jun 2017

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top