Mkurugenzi Mtendaji wa programu ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mazingira amesema muungano wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi hautavunjika, kufuatia uamuzi wa Marekani kutaka kuvunja ahadi ya makubaliano ya Paris.
Eric Solheim ameiambia BBC kwamba China na Ulaya kwa sasa zimeshika usukani na India zimekuwa zikifanya kazi kubwa, hivyo madhatra yatakayotokana na uamuzi wowote utakaochukuliwa na Rais Donald Trump hautakuwa na umuhimu kushinda ilivyokuwa wakati mkataba huo ukisainiwa mwaka 2015.

Rais Trump wa Marekani amesema atatangaza uamuzi wake juu ya azimio hilo la Paris baadaye leo.
China na Umoja wa Ulaya wanajiandaa kutoa taarifa ya pamoja kuunga mkono mkataba huo.
Chapisha Maoni