Baadhi ya wauza nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin

Sherehe ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku mwaka huu.

Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.

Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.

Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa.

Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.Wateja wa nyama ya mbwa wakibugia vipande vya nyama ya mbwa katika sherehe ya Yullin ya mwaka uliopita

Siku ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.

Mwanaharakati mmoja aliambia BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa.

Katika sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangiwa kuchinjwa.

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top