Image result for MAGUFULI LEO ZIARA
Rais John Magufuli ameanza ziara ya siku tatu mkoani Pwani ambako amewatangazia neema wakazi wa mkoa huo kwa kuwaahidi kujenga bandari kavu eneo la Ruvu ambayo itakuwa ikipitisha mizigo ya nchi jirani.
Pia amesema ataendelea kuhakikisha anakuwa upande wa Watanzania wanyonge na kutatua changamoto ambazo zinasababishwa na viongozi wenye tama na wanaotumia vibaya rasilimali za taifa.
Amesema kwa utajiri uliopo Tanzania haikupaswa kuwa nchi masikini, hivyo atahakikisha anashughulika na baadhi ya viongozi wenye tamaa na wanaotumia rasilimali za taifa vibaya.
“…nitalala nao mbele kwa nguvu zangu zote, nitalala nao mbele kwa kumtanguliza Mungu ili kusudi maisha ya Watanzania hawa yabadilike. Nitakuwa upande wa wananchi wanyonge,” amesema Rais Magufuli.
Ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kwanza na wananchi  mkoani humo ambapo amesema kuwa, ujenzi wa bandari hiyo ni fursa kubwa kwa wakazi wa Ruvu na kwamba serikali inafanya hayo kwa ajili ya wananchi wake.

“Lakini pia itajengwa barabara ya kisasa “Express way’ itakayotoka Dar es Salaam kwenda Chalinze ambayo itakuwa na njia sita pamoja na barabara za juu, na hayo ndio maendeleo,” amesema Rais Magufuli. Ameongeza kuwa Tanzania ni nchi tajiri, hivyo ni lazima wananchi wake wawe na maisha ya kitajiri badala ya kuwa matajiri na kuwasindikiza watu wengine katika utajiri huo.

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top