Biashara hiyo ilikamilishwa katika mkutano mjini Washington kati ya waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatari.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBiashara hiyo ilikamilishwa katika mkutano mjini Washington kati ya waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatari.
Qatar imetia saini mkataba wa thamani ya dola bilioni 12 kununua ndege za kivita aina ya F-15 kutoka Marekani.
Biashara hiyo ilikamilishwa katika mkutano mjini Washington kati ya waziri wa ulinzi nchini Marekani Jim Mattis na mwenzake wa Qatari.
Hatua hiyo inajiri siku kadhaa baada ya rais Donald Trump kuishutumu Qatari ,mshirika mkubwa wa Marekani kwa kufadhili ugaidi wa kiwango cha juu ,madai ambayo Qatar imekana.Mataifa mengine ya Ghuba hivi karibuni yalivunja uhusiano wao na Qatar wakiilaumu nchini hiyo kwa kuliyumbisha eneo hilo kupitia ufadhili wake wa makundi yenye itikadi kali na uhusiano wake na Iran.
Qatar ndio taifa lenye kambi kubwa ya majeshi ya Marekani katika eneo la mashariki ya kati ,Al-Udeid .
Ramani ya Qatar inayoonyesha nchi zilizokata uhusiano na taifa hilo
Image captionRamani ya Qatar inayoonyesha nchi zilizokata uhusiano na taifa hilo
Kambi hiyo ina takriban wanajeshi 10,000 na ni muhimu katika operesheni za marekani dhidi ya kundi la Islamic state nchini Syria na Iraq.
Matamshi ya rais Trump yalienda kinyume na idara ya ulinzi nchini humo ambayo ilikuwa imeisifu Qatar kwa kuendelea kuimarisha usalama wa kieneo siku chache awali.
Saudia ambaye pia ni mshirika mkuu wa Marekani imeongoza hatua za kutaka kulitenga taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa gesi kuanzia mapema mwezi huu.
Riyadh ilifunga mpaka na anga yake kwa ndege za Qatar Airways huku Bahrain ,UAE na Misri zikivunja uhusiano wao wa kidiplomasia na taifa hilo.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top