Viongozi wa juu wa Chadema, Freeman Mbowe na Edward Lowassa wameupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo.
Ndesamburo alifariki ghafla wiki iliyopita wakati akipata matibabu katika hospitali ya KCMC.
Mwili wa Ndesamburo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi Mjinim,utaagwa katika viwanja hivyo na leo saa kumi jioni utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga Ndesamburo.
Matukio mbalimbali kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye msiba wa Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo aliyefariki hivi karibuni mkoani humo, Marehemu Ndesamburo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini utaagwa kwenye uwanja wa Majengo kuanzia leo na kesho na kisha kuzikwa mkoani humo haya ni matukio kadhaa ya picha za matukio yanayoendelea katika msiba huo.
Baadhi ya wa vijana waendesha bodaboda wakijiandaa kwa ajili ya maandamano maalum wakati mwili wa marehemu utakapokuwa akipelekwa kwenye uwanja wa Majengo.
Gari Maalum litakalochukua mwili wake.
Chapisha Maoni