Screengrab purportedly showing a Nato fighter jet close to a Russian plane carrying the defence ministerHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNdege ya Nato yaikaribia ile ya waziri wa Urusi Baltic
Ndege ya jeshi la NATO imeikaribia ndege ya Urusi iliyokuwa imembeba waziri wa ulinzi wa Urusi lakini ikafukuzwa na ndege ya jeshi la Urusi iliyokuwa ikiisindikiza ndege hiyo.
Vyombo vya habari vilisema kuwa kisa hicho kilitokea katika anga ya kimataifa eneo la Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda himaya ya Urusi ya Kaliningrad.Nato baadaye ilisema ilifuatilia ndege za Urusi lakini haakujitambulisha.
Mapema Marekani ilisema kuwa ndege ya jeshi la Urusi iliikaribia ndege ya ujasusi ya Marekani umbali wa mita 1.5.
Map
Image captionKisa hicho kilitokea katika anga ya kimataifa eneo la Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda himaya ya Urusi ya Kaliningrad.
Lakini Urusi ilisema kuwa ndege hiyo ya ujasusi ilikuwa imefanya uchokozi.
Visa kadhaa kama hivo vimeripotiwa miaka michache iliyopita huku Nato na Urusi wakilaumiana.Kulingana na mashirika ya habari ya Urusi ndege ya F16 ilipita karibu na ndege ya Shoigu.
Yanasema kuwa kisha ndege ya Urusi ya Su-27, ikaingilia kati na kutoa ishara kuonyesha kuwa ilikuwa imejihami.
Kisha ndege ya Nato ikaondoka.

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top