qatar
Image captionshirika la ndege la Qatar
Mgawanyiko kati ya nchi ya Qatar na nchi kadhaa za jirani huenda ukasababisha kuongezeka kukatizwa kwa safari za anga.
Saudi Arabia, Bahrain na Misri wamethibitisha kwamba nao watasitisha safari za anga kuelekea Qatar kuanzia leo.Mashirika makubwa ya anga ya kikanda, ikiwemo Emirates na Etihad, ni miongoni mwa mashirika yatakayo sitisha safari za anga nchini humo.
Qatar imekanusha madai kwamba inasaidia watu wenye msimamo mkali na kuyaita madai hayo kama upotoshaji kamili.Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba mzozo huo hautaathiri chochote katika utaratibu wa maisha , ingawa kuna taarifa za wananchi kuanza kuhifadhi chakula kama dharula tangu mzozo huo ulipoibuka siku ya Jumatatu wiki hii.
Nchi ya Saudi Arabia tayari imekwisha tangaza kufungwa kwa mpaka pekee wa aridhini na Qatar
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top