Image result for msanii roma mwalimu
Mkali wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’.

MKALI wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ anatarajiwa kuwa mwalimu wa muda wa somo la hisabati leo  katika Shule ya Msingi, Mchikichini iliyopo Mbagala-Kibondemaji jijini Dar es salaam.



Akizungumza na Showbiz Xtra , Roma anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Viva R.O.M.A Viva, K, Ivan na Kaa Tayari alisema kuwa, ameamua kuchukua nafasi hiyo kwanza kujikumbushia kazi yake ya ualimu aliyokuwa akiifanya zamani ambapo alikuwa mwalimu mzuri wa somo la hisabati.

“Somo la hisabati ni miongoni mwa masomo yanayotengwa sana na wanafunzi wengi hivyo basi nikiwa kama mwalimu niliyepitia kufundisha somo hili, nimeona vyema kuhamasisha wanafunzi walipende na kuliamini. “Nitagawa vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba na pia kuwafundisha somo hilo. Kila mmoja nitahakikisha amehamasika na somo hili na kulipenda kama masomo mengine,” alisema R.O.M.A.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top