HOTUBA ya Bajeti ya Serikali pamoja na taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2017/18 inasomwa Alhamisi wiki hii bungeni mjini hapa, huku ikitarajiwa kujikita katika maeneo makuu saba.
Ratiba ya shughuli za Mkutano wa 7 wa Bajeti, inaonesha kwamba bajeti ya serikali itasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, ambapo asubuhi 4.30 itasomwa taarifa ya hali ya Uchumi na jioni saa 10.00 bajeti ya serikali. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango mapema Machi 29, mwaka huu, bungeni mjini Dodoma, alisoma mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 .
Waziri Mpango alisema, Serikali katika bajeti ya mwaka huu 2017/18 inatarajia kuwa na ukomo wa Sh trilioni 31.6. “Kati ya fedha hizo za maendeleo zimeongezeka kutoka Sh trilioni 11.8 katika mwaka 2016/2017 hadi Sh trilioni 11.9 katika mwaka huu wa bajeti 2017/2018, ongezeko hilo ni kiasi ni sawa na asilimia 38 katika bajeti hiyo tarajiwa. Waziri Mpango aliwasilisha, mapendekezo hayo bungeni siku chache kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge la 11, Aprili Mosi mwaka huu.
Akisoma mapendekezo ya bajeti ya 2017/18 Dk Mpango alisema, maeneo ya kipaumbele ni miradi ya maendeleo inayolenga kufanikisha utekelezaji wa Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. “Miradi ya maendeleo ni pamoja na ule wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga, ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam, Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa kilomita 1,251 kwa kiwango cha standard gauge,” alisema na kuongeza: “Ujenzi huo ni pamoja na matawi ya Tabora kupitia Isaka hadi Mwanza (kilometa 379), Isaka hadi Rusumo (kilometa 371), Kaliua kupitia Mpanda hadi Karema (Kilometa 321), Uvinza toka Hoima, Uganda hadi Tanga,Tanzania na kusomesha vijana wengi zaidi katika stadi za mafuta na gesi pamoja na uhandisi na uboreshaji huduma za afya,” alisema na kuongeza: “Maeneo mengine ni viwanda vya kukuza uchumi wa viwanda, kuwianisha maendeleo ya uchumi na ya watu na mazingira ya wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji,” alisema.
Waziri Mpango alisema, eneo lingine muhimu ni uendelezaji sekta za ubia kati ya sekta ya umma na binafsi pamoja na maeneo mengine muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa. Dk Mpango alisema, lengo la uandaaji wa mpango wa bajeti, unaongoza serikali katika kusimamia mambo ya uchumi ikiwamo kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa kufikia asilimia 7.5 katika mwaka huu, asilimia 7.9 mwakani na asilimia 8.2 mwaka 2019.
“Mpango huo unalenga kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kubaki na tarakimu moja hadi kufikia asilimia 5.0 katika kipindi cha muda wa kati, kuwa na pato ghafi la taifa la Sh trilioni 123.9 kwa mwaka 2017/18, Sh trilioni 139.7 kwa mwaka 2018/19 na Sh trilioni 165.4 mwaka 2019/20. Pia mapato ya kodi kufikia asilimia 14.6 ya pato la taifa mwaka 2017/18, asilimia 15.5 mwaka 2018/19 na asilimia 15.8 mwaka 2019/20.
Dk Mpango alisema sura ya bajeti ya serikali mwaka huu 2017/18, ni Sh trilioni 32 zitakazokusanywa na kutumika katika kipindi hicho, mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh trilioni 20.872 sawa na asilimia 63 ya mahitaji yote. Kati ya mapato hayo, serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya Sh trilioni 18.097 sawa na asilimia 87 ya mapato ya ndani na mapato yasiyo ya kodi Sh trilioni 2.022 na kutoka vyanzo vya halmashauri yanatarajiwa kuwa Sh bilioni 753.3.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, serikali inategemea kukopa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 900 (Sh trilioni 2.080 kutoka vyanzo vya nje vyenye masharti ya kibiashara na Sh trilioni 4.434 zinazotarajiwa kupatikana kutokana na mikopo ya ndani kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za serikali zinazoiva. Kwa mujibu wa waziri huyo, Sh trilioni 1.859, sawa na asilimia 1.5 ya Pato la Taifa ni mikopo mipya ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Pia washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh trilioni 3.7. Kati yake, Sh bilioni 496.3 ni misaada na mikopo nafuu ya kibajeti (GBS), Sh trilioni 2.821 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo na Sh bilioni 382.4 ni misaada na mikopo nafuu ya mifuko ya pamoja ya kisekta. Dk Mpango alisema, serikali inapanga kutumia Sh trilioni 32.946 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo, kati yake, Sh trilioni 19.782 zitatengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo Sh trilioni 7.206 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa serikali na taasisi za umma na Sh trilioni 9.723 ni kwa ajili ya kulipia deni la Taifa lililoiva.
Aidha, matumizi ya maendeleo yatakuwa Sh trilioni 13.164, sawa na asilimia 40 ya bajeti yote, ambapo fedha za ndani ni Sh. trilioni 9.960, sawa na asilimia 76. Wananchi waliohojiwa na Habarileo, Juma abdulrahman wa mjini Dodoma alisema, bajeti ya mwaka huu 2017/18 badala ya kutangaza kuongeza bei za bidhaa, vyakula na vinywaji, inatakiwa kuangalia vyanzo vipya vya kodi ili kupata mkusanyo zaidi.
Mdau mwingine wa Mjini Dodoma, Amina Kasian, alisema serikali inatakiwa kuwapunguzia mzigo wananchi kwa kuachana na kupandisha vinywaji kama soda na bia na sigara, inatakiwa kuanza kutafuta vyanzo vingine vya kuongeza mapato ya serikali. Kwa mujibu wa ratiba ilitolewa na Ofisi ya Bunge inaonesha kwamba kila siku kutatanguliwa na maswali na majibu na baadaye kufuata shughuli nyingine ikiwamo ya serikali kushauriana na Kamati ya Bajeti ili kufanya majumuisho kwa kuzingatia hoja zenye maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili bajeti za wizara ikiwamo kuongezewa fedha wizara ya maji na umwagiliaji.
Wiki hilo litahitimishwa kwa wabunge kusoma na kutafakari hali ya uchumi na hotuba ya bajeti hiyo na mjadala wake utaendelea utaendelea kwa siku saba hadi Jumanne Juni 20, ambao mtoa hoja atahitimisha na Bunge zima kupigaji kura ya wazi na ndiyo siku ambayo muswada wa sheria ya fedha za matumizi utawekwa mezani. hadi Kelema kwenda Musongati (kilometa 203),” alisema.
Dk Mpango alisema, miradi mingine ya uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ujenzi wa mitambo ya kusindika gesi mkoani Lindi na Mtwara, uanzishwaji wa Kanda Maalumu za Kiuchumi mkoani Tanga, Bagamoyo, Kigoma na Ruvuma. “Uanzishwaji wa kituo cha biashara cha Kurasini Dar es Salaam, bomba la mafuta ku-
Chapisha Maoni