Rais ameyasema hayo leo wakati akizindua mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki jijini Dar es Salaam ambapo Rais, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar walipewa Ipad maalum zitakazowawezesha kufuatilia ulipaji kodi utakavyokuwa ukifanyika.
Katika hotuba yake Rais Magufuli alisema kuna wafanyabiashara ambao sio waaminifu na kusema uongo kuwa wanapata kipato kidogo kwa lengo la kulipa kodi kidogo, ilhali wanapata kipato kikubwa na kuamua kuiibia serikali kwa makusudi.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli wote hao dawa yao ni Data Center (Kituo cha ulipaji kodi kielekroniki) ambao hawatakuwa na njia nyingine zaidi ya kulipa kodi kwa wakati na kwa kiwango stahili.
Amesema anapenda sana ubinafsishaji kwa ujumla na kuwaomba wananchi wasimuelewe vibaya kuhusu ubinafsishaji "Watu wasinielewe vibaya kuwa nachukia ubinafsishaji, lakini ubinafsishaji wa hovyo nauchukia kwelikweli” amesema Dk Magufuli kwa msisitizo.
Chapisha Maoni