Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Mataifa ya Milki za Kiarabu (UAE), Libya na Yemen yamekata uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar.
Lakini je, hili linatoa maana gani kwa uchumi wa Qatar, na kwa watu wanaofanya biashara huko?
Qatar ina watu milioni 2.7, na ni taifa dogo katika eneo la kaskazini mashariki mwa pwani ya rasi ya Arabia, ambalo linaonekana kujaribu kupigana na wenye nguvu kuishinda. Unaweza kusema ni kama mwanadamu kushindana na ndovu.
Wengi wanalifahamu taifa hilo kutokana na kuwa na shirika kubwa la ndege linalofanya safari zake katika mataifa mengi duniani - Qatar Airways- , pamoja na shirika kubwa la habari duniani -Al Jazeera.
Mbali na hayo, Qatar ilishinda kuwa mwenyeji wa kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia la Dunia mwaka 2022, na pia kuwa mfadhili mkuu wa klabu maarufu sana ya soka Duniani, Barcelona.
Na kwa sababu ya kuwa na uwanja mkubwa sana na maaarufu wa ndege katika mji wake mkuu Doha, nchi hiyo imefaulu kuvutia mashirika makubwa duniani kufungua afisi zake jijini humo.
Kwa hivyo hatua hii ya hivi punde, ina uzito mkubwa sana.Shirika la ndege lenye makao yake makuu Abu Dhabi- Etihad Airways na lile la Dubai, Emirates, yote mawili yanasitisha safari zake zote kuingia na kutoka Doha, kuanzia Jumanne asubuhi.
Mashirika hayo yote mawili, hufanya safari nne za ndege kila siku kuingia na kutoka Doha.
Shirika la safari za bei nafuu la FlyDubai, pia linafutilia mbali safari za kwenda Doha, kwa pamoja na mashirika mengine ya ndege, yakiwemo Bahrain Gulf Air, huku Egyptair ikitazamiwwa kufuata mkondo huo.
Hatua hiyo inatukia baada ya Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri kutangaza kuwa, zinasitisha safari zake za ndege za kuingia na kutoka Qatar, huku pia yakifunga anga zake kutoruhusu ndege za Qatar Airways kupaa.
Kwa hali hii bila shaka ni Qatar Airways ndilo shirika litakalopata hasara kubwa.
Kwa upande mmoja, safari za ndege zake zinazoelekea maeneo kama Dubai, Abu Dhabi, Riyadh na Cairo zitasitishwa.
Na hiyo ni safari kadhaa za kila siku.
Tayari kampuni hiyo imetangaza kuwa inafutilia mbali huduma zakee za usafiri huko Saudia.
Lakini pia marufuku ya kuruka katika anga za mataifa kadhaa kwwenye maeneo hayo pia, itasababisha changamoto kubwa, na kuilazimisha kuyumbisha njia zake za usafiri wa angani, huku ikiongeza muda kwa baadhi ya safari kwa mataifa mengine ambayo imesalia.
Italazimisha pia kuongezwa kwa nauli, hatua itakayowakasirisha abiria wa maeneo mengine.
Ukuaji wa Qatar Airways, umekuwa taratibu baada ya kujiweka katika nafasi bora ya kuwa kampuni tajika ya usafiri wa ndege inayotegemeewa na wengi, katika kuunganisha mataifa ya Bara Asia, Uropa kupitia Doha.
"ikiwwa safari ya kuelekea Ulaya ilikuwa ikichukua masaa 6, sasa itachukua kati ya masaa 8 au 9, kwwa sababu ya kubadilisha mkondo, na hilo halitawafurahisha abiria wengi, na wanaweza kutumia usafiri mbadala," anassema Ghanem Nuseibeh, mshauri mkuu wa kampuni ya Cornerstone Global.
Chakula
Mataifa ya jangwani, kwa hali zao, yanajaribu kila mbinu kupanda chakula.
Usalama wa chakula kwa mfano ni tatizo kuu huko Qatar, kwani inapakana na taifa pekee Saudi Arabia katika eneo la ardhi.
Kila siku mamia ya malori huvuka mpaka na chakul, ambayo ndiyo mzigo mkuu unaosafirishwa.
Karibu asilimia 40% ya chakula cha Qatar inaaminika kupitia njia hiyo.
Na sasa Saudi Arabia imetangaza kufunga mpaka huo wake, na ikiwa barabara hiyo ya ardhini itazuiwa, bila shaka Qatar itategemea usafiri wa angani na baharini.
"Hatua hiyo moja kwa moja itasababisha mfumuko wa bei, na hiyo itawaaadhiri vibaya raia wa kawaida wa Qatari," anasema Bw. Nuseibeh.
Huku akiongeza, "ikiwa bidhaa zitaanza kuuzwa kwa bei ya juu kuliko ilivyokuwa, hapo tutaanza kuwaona wa- Qatari, wakianzisha shinikizo la kisiasa, kwa familia inayoongoza kwa aidha kubadilisha uongozi au mkondo wa kisiasa."
Pia anaeleza kuwa jamii nyingi maskini ya wa-Qatari, wanasafiri kila siku au kila wiki hadi Saudia kwenda kununua bidhaa ya shambani, kwani inauzwa kwa bei nafuu huko.
Ujenzi
Taarifa mpya inaonesha kuwa, sekta ya matibabu, miradi ya usafiri wa treni na ujenzi wa viwanja vinane vikuu vya michezo vitakavyotumika katika mashindano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2022, ndio pekeee baadhi ya miradi mikubwa ya ujenzi inayoendelea kwa sasa nchini Qatar.
Vifaa vikuu vinavyotumika ni mawe na simiti pamoja na chuma, ambayo huingizwa nchini humo kwa kutumia usafiri wa majini na pia ardhini ambapo meli ya mizigo na malori makubwa huingia kutokea nchi jirani, Saudia Arabia.
Hatua ya kufungwa mpaka huo, kutafanya ongezeko la bei ya chakula na kuchelewa kwa bidhaa kufika.
Ukosefu wa pembejeo katika sekta ya ujenzi, kunaweza kufanya hali kuwa hata mbaya zaidi.
Muda mrefu wa kuendelea kufunga anga na mipaka ardhini, kutasababisha hali mbaya hata kutatiza muda na tendakazi katika maandalizi ya kombe la Dunia, anasema Kristian Ulrichsen, mtaalamu mmoja kutoka Ghuba la Uajemi anayefanya kazi katika taasisi ya Baker nchini Marekani.
Watu
Hatua ya kusitisha ushirikiano wa kidiplomasia na kuwazuia raia wa Saudia, UAE na Bahraini kusafiri hadi Qatar, kuishi au kupitia nchi hiyo, ni kwa mjibu wa taarifa kutoka utawala wa Saudi.
Watu wanaotatizika na ilani hiyo wana siku 14 tu kuondoka.
Wakati huo huo, Wa- Qatari, wana muda sawa na huo, kuondoka Saudi Arabia, UAE na Bahrain.
Na hali itakuwa hata mbaya zaidi ikiwa Misri pia itaidhinisha marufuku.
Kwwa mjibu wa ripoti ya hivi majuzi, zaidi ya wa-Misri wapatao 180,000, wanaishi Qatar - ambapo wengi wanajihusisha na kazi za uhandisi, matibabu, sheria na ujenzi.
Kupotea kwa wafanyikazi, kutasababisha matatatizo makubwa kwa kampuni za nchi hiyo pamoja na za kimataifa zinazofanya kazi katika taifa hilo la Ghuba.
Biashara
Tayari tunaanza kuona maafikiano ya kibiashara yakianza kuporomoka.
Kampuni nyingi huko ghuba, zimo nchini Qatar, zikiwwemo zile za reja reja.
Kuna uwezekano kuwa maduka hayo makubwa makubwa ya biashara za reja reja, yakafungwa, kwa muda, anaamini Bw. Nuseibeh.
Timu kubwa ya kandanda huko Saudia, Al-Ahli yamefutilia mbali mkataba wa ufadhili na Qatar Airways.
Chapisha Maoni