Kiranja wa walio wengi Bungeni Steve ScaliseHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKiranja wa walio wengi Bungeni Steve Scalise

Kiranja wa walio wengi katika Bunge la Congress nchini Marekani Steve Scalise, amepigwa risasi na kujeruhiwa alipokuwa akihudhuria mazoezi ya mchezo wa baseball miongoni mwa wabunge.
Yamkini watu wawili wamejeruhiwa, katika kile mashuhuda wanasema kuwa kisa cha umiminunaji wa risasi katika jimbo la Virginia mapema leo Jumatano.
Seneta wa Republican, Rand Paul, anasema kuwa alisikia mlio wa risasi ya kwanza, kisha ikafuatiwa na milio ya risasi.
Walinda usalama walijibu mashambulio hayo.


Ramani ya Jimbo la Virginia
Image captionRamani ya Jimbo la Virginia

Bwana Scalise ambaye ni mwanachama wa chama cha Republican, anasemekana alipigwa risasi kwenye makalio, huku ikisemekana kuwa afya yake haimo hatarini kwani amefikishwa hospitalini kwa matibabu pamoja na walinzi wake ambao pia walijeruhiwa na mshambuliaji.
Idara ya Polisi huko Virginia, inasema kuwa imemtia mbaroni mshambuliaji.


Mbunge Ruben Kihuen‏ aliweka kwenye mtandao wa tweeter picha hii ya wabunge wa Democratic, wakiwaomba manusura wa mshambuliaji huyoHaki miliki ya picha@REPKIHUEN
Image captionMbunge Ruben Kihuen‏ aliweka kwenye mtandao wa tweeter picha hii ya wabunge wa Democratic, wakiwaomba manusura wa mshambuliaji huyo

Rais Donald Trump amesema kuwa: "Tumetamaushwa mno na janga hilo."
Katibu wa mawasiliano wa Ikulu ya White House , Sean Spicerameandika katika mtandao wa kijamii wa tweeter kuwa Rais Donald Trump anajulishwa kuhusiana na shambulio hilo.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top