Kanisa moja katika mji mkuu wa Ghana, Accra, limeandaa ibada ya kutoa shukrani kutokana na ufanisi wa hivi majuzi wa Chelsea katika Ligi ya Premia.
Mchungaji Azigiza ambaye ni shabiki damu wa klabu hiyo aliwahamisha waumini wafike kwa ibada wakiwa wamevalia fulana za klabu hiyo.
Alisimama juu ya keki ya Chelsea kwenye jukwaa ambalo lilikuwa limejengwa kufanana na uwanja wa soka.
Alisema: "Chelsea, kwa kudura zake Mungu, walimaliza wa kwanza."
Aliambia BBC kwamba alitaka kutumia nguvu za soka kuzungumzia kuhusu Mungu.
Azigiza pia aliongoza waumini kuimba aya ya wimbo wa klabu ya Chelsea, Blue is the Colour.
Pasta huyo, ambaye wakati mmoja alikuwa DJ wa redioni, alikuwa pia anamtania mkuu wake katika kanisa hilo la Living Streams International Church, Pasta Ebenezer Markwei, ambaye ni shabiki wa Arsenal, na ambaye alikuwa amemkaribisha kwa ibada hiyo
Pasta Markwei alitoa mahubiri kuhusu "mema, mabaya na maovu ya ushindani" akidokeza kwamba mashabiki wa soka wanafaa kushiriki katika ushindani mwema.
Alisema kuna mambo mema sana katika kfuurahia ufanisi wa watu wengine.
Chelsea walishindwa na Arsenal 2-1 katika fainali Kombe la FA.
Chapisha Maoni