Rais Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton ikulu mjini Dar es Salaam.Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionRais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu nchini humo.
Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania inasema imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake nchini humo.
Taarifa kutoka ikulu inasema hayo ni miongoni mwa mambo ambayo yameafikiwa katika mkutano kati ya Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation Prof. John L. Thornton na Rais John Magufuli.
Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.Image result for mtambo wa kuchenjulia dhahabu
Mazungumzo kati ya wawili hao yalihudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi.
Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu nchini humo.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top