Shirikisho la soka duniani Fifa limetetea mfumo mpya wa teknolojia ya Video uliobuniwa kuwasaidia Marefa kutoa maamuzi sahihi (VAR) kuwa teknolojia hiyo itafaa sana katika mchezo wa mpira wa miguu siku za mbeleni
Lengo shirikisho hilo la soka ni kuona teknolojia hiyo inatumika katika fainali za michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 ambazo pia zitachezwa Nchini Russia.
Rais wa Fifa Gianni Infantino amesema : "Tumeona namna teknolojia hii ya video inavyoweza kuwasaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi uwanjani.
Katika maelezo ya Fifa katika matukio matano yaliyotokea kwenye michuano ya kombe la mabara yakaamuliwa na teknolojia hiyo imeonyesha manne ni ya kuzidi na moja ni la mchezaji kushika mpira.
Gianni Infantino anataka Majaribio ya VAR yafanikiwe ili teknoloji hiyo ipitishwe kuweza kutumika rasmi katika fainali zijazo za kombe la dunia.
Chapisha Maoni