Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba basi la Wibonela Express lenye namba za usajili T158 CEX lililokuwa linatoka Dar es salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyanga limegongana na basi la Tak-biir lenye namba za usajili T818 CYQ katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma ambapo ujenzi wa barabara unaendelea.


Taarifa za awali zinasema watu kadhaa wamejeruhiwa.

Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi la Wibonela wanasema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wao ambaye alikuwa anaendesha basi kwa mwendo kasi na hakujali malalamiko ya abiria wake kila walipomwambia apunguze mwendo.

"Hii ni mara ya pili,ya kwanza tulinusurika kupata ajali,alikuwa anaovatek 'anajaribu kuyapita magari mengini' bila  kuchukua tahadhari,ukiwaambia wanakuwa wabishi",wamesema.
 Tutawaletea taarifa kamili hivi punde
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top