Abas Abdullahi Sheikh
Image captionAbas Abdullahi Siraji alikuwa waziri wa umri mdogo zaidi Somalia
Mwanajeshi wa Somalia aliyempiga risasi na kumuua waziri wa umri mdogo zaidi aliyewahi kuteuliwa nchini Somalia amekuhukiwa kuuawa kwa kupigwa risasi.
Abas Abdullahi Siraji aliuawa mwezi uliopita akiwa ndani ya gari lake karibu na ikulu ya rais mjini Mogadishu.
Anadaiwa kuuawa na Ahmed Abdullahi Abdi, aliyemdhania kuwa mwanamgambo wa Kiislamu kimakosa.
Wengi walighadhabishwa na kuuawa kwa waziri huo.
Mahakama ya kijeshi imemhukumu kifo mwanajeshi huyo, lakini anaweza akakata rufaa.Mawakili wa mwanajeshi huyo wanasema mauaji hayo yalikuwa ajali, shirika la habari la AFP limeripoti.
Wanasema gari la waziri huyo liliwafanya walishuku kutokana na hali kwamba lilikuwa linalifuata gari la mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, ambaye mwanajeshi huyo alikuwa anamlinda.
Car with bullet holeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionThe minister was in his vehicle near the presidential palace when he was shot
Siraji, 31, aliibuka kuwa mbunge wa umri mdogo zaidi katika bunge la Somalia Novemba mwaka jana kabla ya kuchaguliwa kuwa waziri wa ujenzi mapema mwaka huu.
Aliishi kama mkimbizi nchini Kenya na alikuwa mfano wa kuigwa na alienziwa na wengi kutokana na bidii yake na kujitolea kufanikiwa.
Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo alimteua kuwa waziri.
Baada ya kuuawa kwake, rais alikatiza ziara yake Ethiopia na kurejea nyumbani kuhudhuria mazishi yake.
Burial of Abas Abdullahi Sheikh
Image captionRais Farmajo alihudhuria mazishi ya Farmajo

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top