Yanga imepangwa kufungua na mabingwa wa Kenya, Tusker, Juni 5. Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema baadhi ya wachezaji wa timu yao ya vijana watachanganywa na baadhi ya wale wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo mipya.
“Kuna wachezaji wamejiunga na timu ya taifa, wengine mikataba yao imekwisha, hivyo wanaweza kusajiliwa kwingine lakini wale watakaobaki watashirikiana na kikosi cha vijana kwa maandalizi,”alisema. kikosi hicho yataanza wakati wowote baada ya kukutana na Kocha Juma Mwambusi ili kumpa taarifa kamili.
Alisema kuna wachezaji wengi wazuri wa timu yao ya vijana ambao watatumia fursa hiyo kuonesha vipaji vyao kwa kushirikiana na wachezaji wazoefu. Mbali na Yanga, wanaoshiriki michuano hiyo timu nyingine za Tanzania ni Simba, Singida United na Jang’ombe Boys ya Zanzibar.
Aidha, timu za Kenya zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards, Tusker na Nakuru All Stars. Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa ligi walifanya ziara Dodoma na Arusha ambapo walirudi Dar es Salaam juzi na wakati wowote wataanza mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo. Bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kucheza na Everton inayocheza Ligi Kuu ya England
Chapisha Maoni