
Kurugenzi ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania TSNP imekusudia kuwasilisha kwa kampuni inayoandaa MISS TZ notisi ya madai na kusudio la kuwafikisha Mahakamani kama watashindwa kuwalipa washindi wa MISS TZ 2016.
Hatua hiyo inakuja baada ya Kurugenzi hiyo kupokea malalamiko kutoka kwa mamiss walioshiriki Miss Tanzania 2016 na kushinda nafasi za 2, 3 na 4 kutolipwa fedha zao walizoahidiwa na waandaaji wa mashindano hayo Lino International Agency Ltd.






Chapisha Maoni