Tanzia : MSANII DOGO MFAUME ALIYEIMBA 'KAZI YANGU YA DUKANI' AMEFARIKI DUNIA



Msanii Dogo Mfaume Enzi za uhai wake



Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia leo 

Dogo Mfaume ambaye alitumbukia kwenye janga la madawa ya kulevya na baadaye kuanza kupata matibabu ya kuondokana na matumizi ya madawa hayo kupitia kituo cha Pilli Missana Foundation kilichopo Kigamboni.

Akiongea na EATV Pili Missana ambaye ni Mkurugenzi wa kituo hicho amethibitisha kufariki kwa msanii huyo.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top