Shinzo Abe amesema anaiheshimu Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionShinzo Abe amesema anaiheshimu Korea Kaskazini
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameishutumu Korea Kaskazini kutokana na majaribio yake ya makombora katika bahari nchini Japan.
Amesema kuwa hata katika mkutano wa G-7 wa hivi karibuni chokochoko za Korea Kaskazini zilijadiliwa kwa uzito mkubwa.
Waziri Abe amesema kuwa Japan itashirikiana na mataifa mengine ikiwemo Marekani kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini.

Ameahidi kuunga mkono makubaliano ya mkutano wa G-7.
Waziri kiranja nchini Japan Yoshihide Suga, anasema kuwa majaribio haya ya makombora ya Korea Kaskazini yanahatarisha shughuli za uchukuzi ndani ya Bahari nchini Japan.
Katika siku za hivi karibuni Korea Kaskazini imekuwa na choko choko dhidi ya Marekani kuhusiana na mpango wake wa nyuklia na hatimaye Japan nayo imeguswa na harakati hizo za Korea Kaskazini.

Mada zinazohusiana

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top