Rais Dk John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia ngazi kwa kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.
Waziri Muhongo ameambiwa ajitathimini na bila kupoteza muda mrefu achukue hatua kutokana na kadhia hiyo.
Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena kukabidhi ripoti yao. Kamati hiyo ya wataalamu wa jiolojia iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.
Akikabidhi ripoti hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Shilingi bilioni 829 hadi trilioni 1.4 kwa makontena yote 277. Endelea kufuatilia tovuti hii kwa habari zaidi.
KWAHABARI MATANGAZO TUPIGIE ;0623372368






Chapisha Maoni