Polisi wa Kuwait wamemkamata njiwa aliyekuwa amebeba dawa za kulevya aina ya Ketamine ambaye alikuwa amenasa kwenye bati la jengo la forodha katika Bandari ya Abdel iliyopo mpakani mwa Kuwait na Iraq.
Katika taarifa iliyoripotiwa na BBC njiwa huyo alikamatwa baada ya kushindwa kuruka baada ya kuzidiwa na uzito wa dawa hizo ambapo alikuwa amebebeshwa kibegi kidogo mgongoni kilichojazwa vidonge 178 vya dawa zinazoaminika kuwa na thamani kubwa akidaiwa kutoka Iraq.
Mbinu hii ya kutumia njiwa katika kusafirisha dawa za kulevya imekuwa ikitumika sana kwenye sehemu zenye ulinzi mkali ambapo mwaka 2015 iliripotiwa kukamatwa kwa njiwa aliyebeba dawa za kulevya aina ya Cocaine na Bangi katika ukuta wa jengo la gereza Costa Rica.
Chapisha Maoni