Gari lililobeba wachezaji wa Ruvu Shooting likiwa limepata ajali




Habari tulizozipata hivi punde ni  kwamba msafara wa timu ya Ruvu Shooting umepata ajali mbele kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea Dar es salaam.

Taarifa kutoka kwa mmoja wachezaji waliokuwapo inasema kwamba gari likiwa katika mwendo tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.

Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata majeraha ya kawaida.
Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde....
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top