Mkataba huo wa NEEC na TSN ni kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyobya Dailynews, Sundaynews, Habari Leo na Spoti Leo.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Beng'i Issa amesema, ushirikiano baina ya NEEC na TSN ni mahususi katika kuchapisha na kutangaza habari za kongamano hilo, na kwamba baraza hilo linaamini katika mtandao mpana, uzoefu na uimara wa kampunivya TSN kupitia mitandao yake ya habari litaweza kuwafikia watanzania wengi wa ndani na nje ya nchi.
"Kongamano hili litakuwa la siku moja na litahusisha uwasilishaji mada na kufuatiwa na ufunguzi rasmi na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim, ambaye pia atatoa zawadikwa washindi waliofanya vizuri katika kupeleka nbele ajenda ya uwezeshaji wananchi kiuchumi," amesema na kuongeza kauli mbiuvya kongamano hilo ni "Wezesha Watanzania Kushiriki Uchumi wa Viwanda". Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi amesema, baraza hilo limepata chombo sahihi katika kuwafikia wananchi na kuwashirikisha kuhusu uchumi wa viwanda.
Amesema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha shughuli kama hizo zinafanikiwa katika kiwango cha juu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa taarifa zinawafikia wananchi kwa wakati. "Kwa ushirikiano huu naamini tutapeleka taarifa kwa wakati muafaka, nashukuru baraza kwa kuchagua kushirikiana na kampuni hii katika masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi," amesema Dk Yonazi.
Aidha, amezikaribisha kampuni na taasisi mbalimbali kushirikiana na kampunibya magazetivya serikali ili taarifa zao ziweze kuwafikia watu wengi zaidi.
Chapisha Maoni