
Mkwe wa rais Donald Trump alijaribu kufanya mawasiliano ya siri na Urusi mwezi mmoja baada ya rais huyo kushinda uchaguzi, vyombo vya habari vimeripoti.
Jared Kushner alitaka kutumia vifaa vya Urusi ili kukwepa kudukuliwa na majususi wa Marekani kulingana na gazeti la The Washington Post na New York Times.
Bwana Kushner ambaye ni msaidizi mwandamizi wa Ikulu ya Whitehouse hajatoa tamko lake.
- Mkwewe Trump aizuru Iraq rasmi
- FBI wamchunguza mkwe wa Trump, Kushner
- Trump amteua mkwe wake kuwa mshauri
Anadaiwa kuchunguzwa na FBI ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wa muingilio wa Urusi kutaka kumsaidia rais Trump kushinda uchaguzi wa Marekani.
Ripoti nchini Marekani zinasema kuwa wachunguzi wanaamini ana habari muhimu ,lakini sio mshukiwa wa uhalifu.
Je, Kushner alifanya nini?
Ripoti za hivi karibuni zilizotaja maafisa fulani wa Marekani kama duru, zilisema kuwa Kushner alizungumza na balozi wa Moscow nchini Marekani Sergei Kislyak, kuhusu kutengeza mfumo mwengine wa mawasiliano kwa kutumia vifaa vya kidiplomasia vya Urusi nchini Marekani.
Mkutano huo ulifanyika mapema mwezi Disemba katika jumba la Trump Tower mjini New York ambalo ndio yaliokuwa makao makuu ya Trump.
Kulingana na ripoti zote mbili, aliyekuwa mshauri mkuu wa bwana Trump Michael Flynn alihudhuria mkutano huo.
Mfumo huo wa mawasiliano ya siri ulihitajika kutumika kuzungumzia kuhusu Syria pamoja na maswala mengine ya sera wakati wa mpito baada ya kuchaguliwa kwa rais Trump mnamo mwezi Novemba hadi wakati wa kuapishwa kwake mnamo mwezi Januari 2017.
Gazeti la Washington Post linasema kuwa pendekezo hilo lilimshangaza bwana Kislyak kwa kua ilimaanisha kwamba Wamarekani wanatumia vifaa vya Urusi katika ubalozi wa Marekani.
Gazeti la New York Times hatahivyo linasema kuwa mfumo huo wa mawasiliano haukuwekwa.
Chapisha Maoni