KIUNGO wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi yake kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 dhidi ya Liberia.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa mwezi ujao na hivyo anatarajiwa kujiunga na timu hiyo kipindi hiki ambacho ligi imekwisha hadi msimu mpya ujao. Kocha wa muda wa Zimbabwe, Norman Mapeza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo huo wa Kundi G dhidi ya Liberia.
Kumusoko anakuwa mchezaji pekee wa Zimbabwe aliyeitwa katika kikosi hicho cha taifa akiwaacha raia wenzake watano wanaocheza ligi ya Tanzania. Kikosi hicho ni makipa; Edmore Sibanda (CAPS United, Zimbabwe), Ariel Sibanda (Highlanders, Zimbabwe), Petros Mhari (FC Platinum) Mabeki: Denis Dauda (CAPS United, Zimbabwe), Partson Jaure, Qadr Amin (both Ngezi Platinum, Zimbabwe), Onesimo Bhasera (SuperSport United), Teenage Hadebe (Chicken Inn, Zimbabwe), Jameson Mukombwe (Black Rhinos, Zimbabwe), Erick Chipeta (Ajax Cape Town), Sydney Linyama (Black Rhinos).
Viungo: Thabani Kamusoko (Yanga SC, Tanzania), Devon Chafa, Ronald Chitiyo (both CAPS United, Zimbabwe), Simon Shoko (FC Platinum, Zimbabwe), Kuda Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns), Marvelous Nakamba (Vittese Arnhem, Holland), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum, Zimbabwe), Ovidy Karuru (AmaZulu). Washambuliaji: Tendai Ndoro (Orlando Pirates), Evans Rusike (Maritzburg United), Knowledge Musona (KV Oostende) na Prince Dube (Highlanders, Zimbabwe).
Chapisha Maoni