April 12, 2025 10:57:45 AM Menu
 
Latest

04:03 AM MMETHALI

Huddersfield Town washerehekeaHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionHuddersfield walimaliza nafasi ya tano katika ligi ya Championship
Klabu ya Huddersfield Town imepandishwa daraja kucheza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza baada ya kulaza Reading 4-3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Wembley Jumatatu.
Baada ya kutoka sare 0-0 dakika 120, Town walitakiwa kupiga mikwaju kwa mara ya pili na walikuwa na bahati tena baada ya kulaza pia Sheffield Wednesday kwa mikwaju ya penalti hatua ya nusufainali.
Christopher Schindler aliwashindia Town baada ya mkwaju wa Liam Moore kupaa angani nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.
Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haijacheza soka ya ligi kuu tangu 1972.
Reading, waliomaliza alama nne na nafasi mbili juu ya Town waliokuwa nafasi ya tano katika ligi ya Championship sasa wameshindwa katika fainali ya muondoano ya kufuzu kwa EPL baada ya ligi kwa mara ya nne.
ReadingHaki miliki ya pichaEMPICS
Image captionReading walimaliza nafasi ya tatu kwenye jedwali ligi ya Championship, alama nne juu ya Huddersfield
Aaron MooyHaki miliki ya pichaPA
Image captionAaron Mooy alikuwa mchezaji bora wa mechi na mmoja wa wachezaji wa Huddersfield waliofunga mikwaju yao Wembley
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
30 May 2017

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top