UWAOKOA
Watoto wafa korongoni na aliyejitosa kuwaokoa
IMEANDIKWA NA SIFA LUBASI, DODOMA IMECHAPISHWA: 03 MACHI 2017
Kuchapa Barua pepe
0 Comments
WATU watatu wamekufa wakiwemo watoto wawili na mtu aliyejitosa majini kuwaokoa baada ya kuzama kwenye maji katika kijiji Suguta wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Katibu Tarafa ya Mlali, Muhsini Mulokozi amethibitisha tukio hilo kuwa ni la Februari 26 mwaka huu saa 11 jioni katika korongo linalotiririsha maji kutoka Kijiji cha Mlali kuelekea kijiji cha Chamkoroma.
Mulokozi ametaja waliopoteza maisha kuwa ni Augustino Nyoni (11) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Suguta, Samson Mbogolo (15) na Julius Mgaisa (35).
Amesema, watoto hao walikuwa wakichunga ng’ombe na wazazi wao ilipofika jioni walisogea katika maji yaliyopo kwenye dimbwi lililopo ndani ya korongo hilo kwa ajili ya kuoga na Mgaisa alipoona nguo juu ya dimbwi hilo na watoto hawaonekani, alikimbia kijijini kutoa taarifa.
“Baada wanakijiji kufika kando ya dimbwi hilo Mgaisa alijitolea kuingia ndani ya maji kwa ajili ya kuwaokoa lakini kwa bahati mbaya naye alifia humo,” ameeleza na kuongeza:
“Nadhani huenda walifikiri kina ni kifupi, lakini baada ya uokozi tumeliona dimbwi ni refu takribani futi 12.”
Amewataka wananchi kuwa makini wanapokuwa maeneo hayo hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mvua nyingi kwani pamoja na maji ya mvua dimbwi lile hupokea maji ya chemichemi zilizopo kijiji cha jirani hivyo halikauki maji masika na kiangazi.
Diwani wa Kata ya Iduo, Valentino Seng’unda amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa kipindi hiki cha mvua, kwa kuwa korongo hilo linajulikana, hivyo ni vyema wawe na msisitizo kwa watoto kuwa ni mazingira hatarishi.
Miili yote ilifanikiwa kuonekana na tayari imeshazikwa.
back to top
Habari_Leo Annivesary
ZILIZOSOMWA ZAIDI WIKI HII
Kichuya kawaumiza tena
Kichuya kawaumiza tena
2017-02-26
Yanga yakiri kuwa na hali ngumu
Yanga yakiri kuwa na hali ngumu
2017-02-28
Mbowe: Mahakama imetufariji sana
Mbowe: Mahakama imetufariji sana
2017-02-28
Yanga: Hatumlazimishi Ngoma
Yanga: Hatumlazimishi Ngoma
2017-03-03
HABARI MPYA
HABARI KUU
SPONSORED LINKS
www.tsn.go.tz
Official Website for TSN
www.dailynews.co.tz
The National Newspaper
www.cardealpage.com
CardealPage Co. Ltd
TUPATE KWENYE FACEBOOK
HALI YA HEWA
Dar es Salaam 30 °C
Dar es Salaam Tanzania Thunderstorms, 30 °C
Current Conditions
Sunrise: 6:28 am | Sunset: 6:41 pm
67% 17.7 km/h 1006.000 in
Forecast
JMM Low: 23 °C High: 32 °C
JMP Low: 24 °C High: 30 °C
JMT Low: 24 °C High: 31 °C
JMN Low: 25 °C High: 31 °C
JTN Low: 26 °C High: 30 °C
ALH Low: 25 °C High: 31 °C
IJM Low: 26 °C High: 31 °C
JMM Low: 25 °C High: 30 °C
JMP Low: 25 °C High: 30 °C
JMT Low: 26 °C High: 29 °C
Mwanza 23 °C
Arusha 23 °C
Dodoma 25 °C
Maskani
Nyota
Breaking News
Kuhusu TSN
Wasiliana Nasi
Tafuta...
Tafuta
Hakimiliki © 2017 HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa. Imetengenezwa na Richard Kazimoto
Chapisha Maoni